Post Top Ad

Jumatatu, 17 Juni 2019

Mohammed Morsi: Utawala wake uliokumbwa na utata ulivyokatizwa na majeshi

Mohammed Morsi alikua rais wa kwanza wa Misri aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia lakini alisalia madarakani kwa mwaka mmoja kabla ya kutumuliwa kupitia mapinduzi ya kijeshi tarehe 3 mwezi Julai mwaka 2013.
Hatua hiyo ya kijeshi ilifuatia maandamano ya siku kadhaa ya kupinga utawala wake na pamoja na hatua ya Morsi kukupuuza amri ya mwisho ya jeshi ya kumtaka asulihishe mzozo mbaya wa kisiasa nchini humo tangu Hosni Mubarak alipong'olewa madarakani mwaka 2011.
Baada ya kuzuiliwa kwa karibu miezi miwili katika sehemu isiyojulikana waendesha mashtaka wa serikali walitangaza mwezi Septemba mwaka 2013 kwamba Morsi atashtakiwa kwa kuwachochea wafuasi wake kumua mwanahabari na wafuasi wawili wa upinzani na kuamurisha wengine kuteswa na kuzuiliwa kinyume cha sheria.
Mashataka dhidi yake yalihusiana na makabiliano kati ya waandamanaji wa upinzani na wafuasi wa kundi la Muslim Brotherhood nje ya makazi ya rais ya Ittihadiya mjini Cairo mwezi Desemba mwaka 2012.
Morsi alishitakiwa pamoja na viongozi wa 14 wa ngazi ya juu wa Muslim Brotherhood Novemba mwaka wa 2013.
Wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake kwa mara ya kwanza, alipiga mayowe kutoka kizimbani akisema kuwa yeye ni mhanga wa "mapinduzi ya kijeshi" na kukataa mamlaka ya mahakama kumfungulia mashtaka.
"Mimi ni rais wa Jamhuri kwa mujibu wa katiba ya nchi na nimezuiliwa kwa nguvu ," alisisitiza.
Lakini mwezi Aprili mwaka 2015, Morsi na washirika wake walihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela baada ya kuondolewa mashtaka ya uchochezi na kupatikana na makosa ya kuamrisha kuzuiliwa na kuteswa kwa waandamanaji.
Morsi pia alifunguliwa mashtaka mengine ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wanamgambo wa kigeni kuwaachklia huru wafungwa wakati wa maandamano ya mwaka 2011, kufichua siri za serikali, ubadhirifu pamoja na kutusi mahakama.

Mbunge wa kundi la Kiislam

Mohammed Morsi alizaliwa katika kijiji cha El-Adwah kilichopo mkoa wa Nile Delta eneo la Sharqiya mwaka 1951.
Alisomea uhandisi katika Chuo Kikuu cha Cairo katika miaka ya 1970 kabla ya kwenda Marekani kusomea PhD.
Aliporejea Misri alikteuliwa mkuu wa kitengo cha uhandisi katika Chuo Kikuu cha Zagazig.
Alishikilia nyadhifa kadhaa katika kundi la Muslim Brotherhood, na hatimae kujiunga na kitengo chake cha kisiasa ambapo aliwania kiti cha ubunge kama mgombea binafsi katika bunge la vuguvugu hilo kutoka mwaka 2000 hadi mwaka 2005
Alipoteza kiti chake cha ubunge nyumbani, kufuatia duru ya pili ya uchaguzi aliyodai ulikubwa na udanganyifu.
Akiwa mbunge alisifiwa sana kwa uweledi wake wa luga na kazi , kwa mfano baada ya mkasa wa reli mwa 2002 alipinga madai ya utepetevu kwa upande wa maafisa wa reli hiyo.
Morsi aliteuliwa kama mgombea wa uraisi wa kundi la mwezi April 2012 naibu kiongozi wake mfanyibiashara Khairat al-Shater, alipolazimishwa kujiondoa katika kinyang'anyiro hicho.
Japo Morsi hakuonekana kuwa na hulka ya msemaji bora alikuwa mwenyekiti wa chama cha Freedom and Justice Party (FJP).
Katika kampeini yake ya uchaguzi, Morsi alijinadi kama mtu atakaeleta mwamko mpya akilinganishwa na viongozi wa zamani kama Hosni Mubarak.

Maandamano mapya

Alipoingia madarakani mwezi Juni 2012 baada ya kushinda uchaguzi kibahati, Morsi aliahidi kuunda "serikali ya Wamisri wote".
Lakini wakosoaji wake walilalamika kuwa alishindwa kutekeleza wajibu wake wakati wa uongozi wake wa mwaka mmoja uliokumbwa na msukosuko.
Walimlaumu kwa kuruhusu makundi yenye misimamo mikali ya Kiislam kuingia katika ulingo wa kisiasa hali iliyoipatia nguvu kubwa kundi la Muslim Brotherhood.
Pia walisema, alivuruga uchumi hali iliyomfanya ashindwe kushughulikia masuala yaliyosababisha maandamano yaliyomleta uongozini: na miito ya kupigania haki na usawa katika jamii.
Upinzani dhidi ya uongozi wa ulianzamwezi Novemba 2012 wakati, azma yake ya kuhakikisaha makundi ya kiislam yanabata wingi wa viti bungeni ili waweze kukamilisha shughuli ya kuandika katiba mpya ili aweze kujipatia mamlaka zaidi
Licha ya maandamano dhidi yake kushika kasi, Morsi alitoa amri ya rais ya kuruhusu vikosi vya usalama kulinda taasisi za kitaifa na maeneo ya kupigia kura hadi kura ya maoni kuhusu katiba mpya ifanyike Disemba 15 mwaka 2012.
Wakosoaji walisema amri hiyo ilikuwa sawa na sheria ya kijeshi ndiposa makabiliano yalizuka kati ya wafuasi wake na upinzani ambapo zaidi ya watu 50 waliuawa.
Maandamano makubwa yalifanywa kuadhimisha mwaka wa kwanza wa utawala wa Morsi, ambapo mamilioni ya watu walijitokeza katika barabara kuu zote nchini Misri.
Mapinduzi'
Majeshi yalitoa onyo kwa Morsi kwamba yataingilia mzozo unaokumba utawala wake ikiwa atashindwa kufikia masharti ya raia katika kipindi cha saa 48.
Ilipofika jioni ya Julai 3, majeshi yalifutilia mbali katiba na kutangaza kubuniwa kwa serikali ya mpito kabla ya kufanyika upya kwa uchanguzi wa urais.
Morsi alipinga hatua hiyo na kuongeza kuwa ni sawa na "mapinduzi".
Alikamatwa kufuatia amri iliyotolewa na mkuu wa majeshi - ambaye ni rais wa sasa- Abdul Fattah al-Sisi - na kupelekwa sehemu isiyojulikana na kwa wiki kadhaa bila ya mtu yeyote kujua hali yake.
Wafuasi wake waliandamana katika barabara za mji wa Cairo, kushinikiza kuachiliwa kwake na kurudishwa madarakani mara moja. 
Majeshi yalijibu hatua hiyo kwa kutumia nguvu kuvunja mandamano mnamo Agosti 14 na kuwakamata vingozi wa wakuu wa vugu vugu la Muslim Brotherhood.
Karibu watu 1,000 waliuawa katika oparesheni hiyo ambayo utawala wa mpito ulidai kuwa juhudi za kukabiliana na"ugaidi".
Miaka iliyofuata baada ya Morsi kuondolewa madarakani, Misri ilishuhudia ongezeko la ghasia na mashambulizi kutoka kwa wanamgambo wa Kiislam na msako mkali dhidi ya vugu vugu Muslim Brotherhood lilitangazwa rasmi kuwa kundi la kigaidi.
Morsi alitoweka machoni mwa umma, na kuishia kuonekana kotini alipofunguliwa mashtaka.
Baadae mtangulizi wake Hosni Mubarak aliachililiwa huru kutoka jela - katika hatua ambayo ilionekana na wengi kuwa Misri haikua imeendelea mbele kisiasa licha ya uchaguzi uliomweka Morsi madarakani kwa muda.

Ads

Post Top Ad

Pages