Akemea maafisa kilimo kukaa Ofisini,kutowatembelea wakulima
Wananchi walalamikia kero ya Maji,mgao wa upendeleo
Watendaji wawekwa kitimoto kujieleza, kujibu maswali
Mkuu wa Mkoa wa Iringa amewataka maafisa kilimo wote kujipima na kuona kama kweli wanaendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano inayotaka kutoka ofisini kuwafuata wakulima na kuhakikisha kero mbalimbali zinazowakabili zinasikilizwa na kupatiwa ufumbuzi.
RC hapi jana ameendelea na ziara yake katika tarafa ya Mazombe ambako amezindua miradi ya maendeleo na kufanya mkutano wa kusungumza na wananchi eneo la Mji mdogo wa Ilula.
Akieleza dhamira ya Iringa mpya, Hapi amekemea tabia ya maafisa wa serikali wakiwemo wale wenye dhamana ya kusimamia kilimo kugeuka kuwa watu wa ofisini na hawatoki kuwafuata wakulima kujua changamoto zao na kuzitatua.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amewataka watendaji wa halmashauri kuchapa kazi kwa malengo ili kuiepusha serikali na lawama ambazo kimsingi wao wanalipwa mishahara kuzitatua.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amewataka watendaji wa halmashauri kuchapa kazi kwa malengo ili kuiepusha serikali na lawama ambazo kimsingi wao wanalipwa mishahara kuzitatua.
Wakieleza kero zao mbele ya Mkuu wa Mkoa, wananchi wa tarafa ya Mazombe wametaja kuwa Mgaka wa Maji wa upendeleo, Umeme, kutosomwa mapato na matumizi pamoja na huduma duni za afya kuwa ndiyo matatizo makubwa wanayokabiliana nayo.
Katika Mkutano huo maarufu kama ‘mahakama ya Wananchi’, kila mkuu wa idara husika ya halmashauri aliwajibika kusimama na kutolea ufafanuzi kero zilizoulizwa na wananchi katika idara yake.
Kuhusu shida ya Maji, RC Hapi amewatoa Shaka wananchi wa Ilula kuwa Serikali ya CCM imeshatenga fedha za mradi wa maji Ilula kiasi cha bilioni 4.9 ambazo zitajenga mradi wa maji, kazi ambayo imeshaanza na inatarajiwa kukamilika mwezi Mei mwaka 2019. Mradi huo ambao RC Hapi ameutembelea, utatatua kero ya Maji mjini Ilula kwa kutoa usambazaji wa sasa wa 47% na kufikisha zaidi ya 87%. Hivyo amewataka wananchi wa Ilula kuwa na subira wakati huu mradi unajengwa.
Aidha, ameagiza wakati Huu mradi unajengwa, mgao wa maji ufanyike kwa uwazi na haki na ratiba ya maji ibadikwe kwenye ofisi zote za vitongoji ili wananchi wajue.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na mradi wa Kiwanda cha nguzo za Umeme, mradi wa Maji Imalutwa Mgombezi na ujenzi wa nyumba za walimu.