jimbo la kaskazini magharibi mwa Nigeria la Kano, wamethibitisha kuwa wanafanya uchunguzi kubaini vi vipi kiasi cha pesa za Nigeria (naira) karibu milioni saba sawa na dola elfu 19 za kimarekani zilipotelea kwenye hifadhi ya wanyama inayojulikana kama Kano Zoological Gardens.
Msamaji wa polisi wa jimbo la Kano, DSP Abdullahi Haruna, ameithibitishia Idhaa ya BBC Pidgin kuwa wanachunguza kisa hicho.
" Ndio ni ukweli pesa zilipotelea kwenye hifadhi ya wanyamaya Kano na pesa hizo zilitakiwa kutumika kwa ajili ya tamasha la siku tano Sallah. Hadi sasa tumekwisha wakamata wafanyakazi 10 wa hifadhi hiyo ya wanyama na wanahojiwa na idara ya upelelezi- CID.
"Miongoni mwa watu waliokamatwa ni mlinzi wa hifadhi ya wanyama, na wafanyakazi wa idara ya fedha na tunataka kufahamu ni kwanini walificha kiasi hicho kikubwa pesa kwenye hifadhi ya wanyama kwa siku tano bila kuzipeleka lkatika benki ," Alisema msemaji wa polisi katika mahojiano.
Jumatano afisa wa mapato ya hifadhi ya wanyama aliripoti kuwa naira milioni sita, laki nane na elfu ishirini zilizopatikana kupitia malipo ya kuwaona wanyama zingetumiwa katika tamasha Sallah na zimetunzwa vema.