Post Top Ad

Jumatatu, 17 Juni 2019

Wema Sepetu: Mahakama ya Kisutu yaagiza ashikiliwe mahabusu siku 7

Mahakama ya kisutu imeagiza msanii maarufu nchini Tanzania Wema Sepetu azuiwe mahabusu hadi Juni 24 baada ya kukiuka masharti ya dhamana katika kesi inayomkabili.
Mahakama imeelekeza kwamba Wema Sepetu azuiwe kwa siku 7 wakati ikisubiriwa kutoa hukumu katika kesi ambapo alishtakiwa kwa kusambaa kwa kanda ya video ya mahaba kati yake na mwanamume mmoja katika mitandao ya kijamii nchini Tanzania.

Wiki iliyopita mahakama ilitoa agizo la kukamatwa kwa nyota huyo aliyekuwa malkia wa urembo nchini.
Waranti ya kukamatwa kwake ilitolewa baada ya mshtakiwa pamoja na mdhamini wake kutofika mahakamani walipohitajika wakati wa kusililizwa ushahidi wa kesi hiyo.
Wakili wa Wema, Ruben Simwanza alieleza kuwa mteja wake alikuwemo mahakamani, lakini aliugua na akalazimika kuondoka - ufafanuzi ambao haukuiridhisha mahakama.
"Kama amekuja mahakamani halafu akaondoka bila kutoa taarifa, mahakama itajuaje kama alikuja? Alishindwa ninikutoa taarifa mahakamani", alisema hakimu.
Wema amewahi kushtakiwa katika kesi nyingine kwenye mahakama hiyo ya Kisutu mnamo 2017 kwa mashtaka ya umiliki wa mihadarati.

Inadaiwa kwamba mnamo tarehe 4 mwezi Februari 2017, Wema na wenzake walipatikana wakimiliki misokoto ya bangi katika eneo la Kunduchi Ununio.
Mahakama ilimpata na hatia Juali 2018 na kumpiga faini ya shilingi milioni mbili za Kitanzania.
Maafisa wa polisi nchini Tanzania walianzisha msako dhidi ya watu maarufu baada ya baadhi yao kuhusishwa na ulanguzi wa mihadarati.

Ads

Post Top Ad

Pages