Breaking

Post Top Ad

Alhamisi, 8 Agosti 2019

Kenya: Wanafunzi wapewa dawa za uzazi wa mpango kuzuia mimba


Kenya: Wanafunzi wapewa dawa za uzazi wa mpango kuzuia mimba

Mimba za utotoni zinachangia 25% ya wasichana kuacha shule katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Saharan Barani Afrika kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia idadi ya watu UNFPA.
Nchini Kenya wasichana 2 kati ya kila wasichana 10 walio na miaka kati ya 15-19 wanaripotiwa kuwa wajawazito au tayari wamejifungua watoto.
Maeneo yalio na idadi kubwa ya mimba za utotoni ni majimbo ya Narok na Kwale Pwani ya Kenya.
Katika eneo la Kwale wazazi wamelazimika kuwapatia mabinti zao wadogo wengine hadi miaka 10 dawa za kupanga uzazi, ili kuwazia wasipate mimba wakiwa shuleni.

Ads

Post Top Ad

Pages