Vagina Museum linalotarajiwa kufunguliwa mjini London litazinduliwa rasmi kwa mara ya kwanza November 16 kufuatia kampeni ya kuchangisha £50,000 kutoka kwa umma.
Jumba hilo linatarajiwa kuelimisha na kutoa uhamasisho kuhusu sehemu hiyo nyeti ya mwanamke na afya ya uke na pia kukabiliana na unyanyapaa.
Muasisi wake analitaja jumba hilo kama " jumba la kwanza duniani linalolenga kuangazia umbo la mwanamke."
Jumba hilo litaangazia maonyesho ya sanaa, michezo ya kuigiza, warsha na pia vichekesho, vyote vikiwa ni kuangazia kuhusu uke.
Mkurugenzi Florence Schechter aliamua kuliidhinisha jengo hilo la maonyesho mnamo 2017 baada ya kugundua Jumba la Phallological lililopo nchini Iceland, linaloonyesha kwa ukubwa uume, na kukosa kujumuisha sehemu hiyo nyeti ya umbo la mwanamke.
Amesema lengo la kufunguliwa jumba hilo la maonyesho London ni "kufuta unyanyapaa kuhusu mwili na umbo la mwanamke" kwa kila mtu haijalishi asili, jinsia au mahusiano.
![]() |
Add captionFlorence Schechter ni mkurugenzi wa jumba hilo la uke |
Bi Schechter amesema jumba hilo ambalo ni la kitamaduni litaendesha miradi kwa watoto katika familia na pia shuleni.
Litaendehsa harakati za kuhakikisha watoto wanajihisi sawa kuzungumzia kuhusu sehemu hiyo nyeti ya mwanamke kuanzia umri mdogo.
"Wanapohisi aibu, inakuwa vigumu kuzungumzia mambo," amesema. "Ni kuhusu kuondoa unyanyapaa kutoka sehemu hiyo ya mwili na kuwa wakweli kuhusu kazi yake."
"Hii ni sehemu ya mwili ambayo watu wanapaswa kujivunia. Jumba hili ni njia nzuri ya kusambaza ujumbe kwamba hakuna sababu ya kuona aibu kuhusu uke."
Jumba hilo 'Vagina Museum' linashirikiana pia na madaktari wa Royal College of Obstetricians na madaktari wengine wa afya za uzazi kwa wanawake kuwashirikisha wanawake katika mjadala kuhusu miiko iliopo kuhusu afya ya wanawake.
Mradi wa jumba hilo utahimiza elimu ya afya na ushirkiano wa tendo la ndoa na itashirikiana na madaktari na wataalamu wa afya kutoa huduma na usaidizi kwa jamii ya watu waliobadilisha jinsia au waliozaliwa na jinsia mbili wasiokuwemo katika kundi la ima wanawake au wanaume.
Zoe Williams, mkurugenzi wa jumba hilo ameiambia TRIPLEE kwamba: "Kufikia sasa kumekuwa na muitikio mzuri sana. Tumeguswa na namna watu wegi wanasema hii ni fikra nzuri."
Bi Schechter ameongeza kuwa jumba hilo la maonyesho ambalo halitolipisha kiingilio, litaruhusu watu wa jinsia tofauti kwasababu "sio kila aliye na uke ni mwanamke, na sio kila mwanamke ana uke"