Post Top Ad

Alhamisi, 19 Septemba 2019

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia


Uganda imesaini makubaliano na Urusi kuisaidia kujenga uwezo wake wa kutumia teknolojia ya nyuklia kwa matumizi ya kutengeneza nishati, dawa na matumizi mengine ya amani.
Hatua hii inafuata kusainiwa kwa makubaliano mnamo mei mwaka jana baina ya serikali ya rais Yoweri Museveni na shirika la kitaifa la nyuklia China CNNC, kulisaidia taifa hilo la Afrika mashariki kuendeleza matumizi ya nishati ya nyuklia kwa madhumuni ya amani.
Katika ujumbe rasmi wa wizara ya nishati Uganda, makubalinao hayo na Urusi yalisainiwa hapo jana Jumatano huko Vienna kati ya waziri Irene Muloni na naibu mkurugenzi mkuu wa shirika la kitaifa la nishati ya atomiki ROSATOM, Nikolai Spasskiy.
  • Urusi itaisaidia Uganda kujenga miundo mbinu ya nyuklia kwa matumizi katika viwanda sekta ya afya na pia ukulima.

"Spasskiy ameeleza uwajibikaji na utayari wa ROSATOM kuisaidia Uganda kuidhinisha matumizi ya amani ya nishati ya nyuklia hususan katika ujenzi wa kinu cha nishati ya nyuklia," taarifa imeeleza hivyo.

Ads

Post Top Ad

Pages