Post Top Ad

Jumanne, 5 Julai 2022

Sopu aliyewapiga hat-trick Yanga atua Azam FC


Club ya Azam FC imetangaza kumsajili Abdul Seleman Sopu kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Coastal Union ya Tanga


Taarifa zisizo rasmi zinadai kuwa Azam FC wamelipa Tsh milioni 100 kukamilisha usajili huo, Sopu ni zao ya kikosi cha dhahabu cha Timu ya Taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys kilichoshiriki AFCON U-17 nchini Gabon.

Sopu ameingia kwenye headlines baada ya kuifunga hat-trick Yanga katika mchezo wa fainali ASFC ambapo Yanga waliibuka Mabingwa kwa penati 4-1 baada ya dakika 120 kumalizika 3-3.

Ads

Post Top Ad

Pages