Kama mungu angenichukua mapema basi nisingeweza leo kuwasimulia mambo haya makuu katika ulimwengu soka katika dunia yenye watu takribani bilion 8.5 ni ngumu sana binadamu wote kuwa sawa ni ngumu sana kila mtu anakuwa na mlango wake wa kuingilia duniani na kuondokea hii ni kama Ibada.
Nayasema haya huku nikiitazama picha ya Juma kaseja kwenye vitabu vyangu vya kumbukumbu bahati nzuri vinanieleza mambo yake mema mengi aliyotutende kwenye Ulimwengu huu hususani katika football yetu hii bado nawaza huku moyo wangu ukimiminika damu nzito yenye asili ya mnyama simba nikikumbuka maisha ya kijana huyu aliyefanya makubwa na jezi ya Simba sports club lakini natamani isiwe kweli nayoyasikia kwenye ngome ya sikio langu..
Nimetazama kwenye vitabu vya Kumbukumbu vya Moro United, Mtibwa Sugar, Simba Sport club,Kuala lampul Malasia(Yanga) bado sikumaliza nikaingia kwenye vitabu vya Mbeya city nikafika mbali zaidi nikaingia mpaka kwenye kabati la watoza ushuru wa kinondoni hapo ndipo nilipo kubali tuache muda uamue unachotaka nipo naendelea kusoma vitabu vyako ulivyooandika na kutuachia kwenye vilabu vyote hivi huku nikiwa na hudhuni tele moyoni sawa Juma nenda nafasi hii finyu niliyoipata ya kuandika mema yako nahisi haitoshi hata kidogo nitaandika wakati mwingine
Pengine hata macho yangu hayawezi kusadiki kweli ninayoisikia machozi yananitoka mithili ya mtoto mchanga pengine ni maumivu nikikumbuka moments zote nilizokuwa nikimtazama Juma K Juma akiwa langoni mwake mikono yangu inasita kuandika miguu yangu inatetemeka kwa hofu nashindwa hata kusimama mithili ya mtu mwenye degedege pengine nashindwa kukubaliana na ukweli halisi kwamba Tanzania One Juma Kaseja amelala Usingizi mzito katika chumba cha peke yake huko nyumbani kwake huku akiota ndoto ndefu ya safari ya maisha yake ya football mpaka mwisho wake pengine yeye ndiye mwenye huzuni kuliko sisi sote kwa sababu pale atakapoamka na kugundua kuwa hayupo nasi