Vyombo mbalimbali vya Habari za Kimichezo kutoka Nchini Uganda na Tanzania vimeripoti Kuwa Klabu ya Simba SC imekubali kutoa Kiasi Cha Dollar 100,000 ambazo ni zaidi ya Shilingi Milioni 233 za Kitanzania kwaajili ya Kumsajili Mshambuliaji hatari,Cesar Manzoki anayekipiga Klabu ya Vipers ya Uganda .
Mwanzo Vipers FC waliitaka Simba SC kulipa kiasi Cha Shilingi Milioni466 lakini wamekubali kupunguza mpaka Shilingi Milioni 233 Baada ya Mchezaji huyo kugoma kufanya mazoezi na timu hiyo huku akishinikiza dili lake na Simba likamilishwe.
.
#NBCPremierLeague