Post Top Ad

Alhamisi, 29 Desemba 2022

Prison watapa milion 30 wakiifunga Simba

 



Kuelekea mchezo wa Simba SC dhidi ya Prisons utakaochezwa Ijumaa ya December 30, 2022 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Mkurugenzi wa Silent Ocean Salaah Said Mohamed kupitia kwa Meneja Masoko wa Silent Ocean Mohamed Kamilagwa ameahidi kuwa ataipa Prisons kiasi cha Tsh. Milioni  30 kama itaifunga Simba SC katika mchezo huo na sare ataipa Tsh. Milioni 10.


“Hawa Vijana wakipewa hamasa wana athari kubwa sana kwahiyo sasa wanakwenda tarehe 30 (vs Simba SC), jana tulikuwa kambini kwao wakijiandaa na sisi tukawaambia Mtendaji Mkuu wetu Salaah Said Mohamed kasema kwamba hawa 

vijana kwa juhudi wanayoifanya akasema kwanini tusiwape Tsh. Milioni 30 wakishinda lakini ikitokea bahati mbaya wakaenda sare wapate Tsh. Milioni 10”


Silent Ocean ni Wadhamini Wakuu wa Tanzania Prisons na wamekuwa na utamaduni wakuwapa motisha Wachezaji wanapocheza mechi, mechi yao dhidi ya Yanga SC walipewa ahadi ya Tsh. Milioni 20 kama wangeifunga na Tsh. Milioni 10 kama wangetoka sare.

Ads

Post Top Ad

Pages