Post Top Ad

Alhamisi, 29 Desemba 2022

Rais wa klabu ya Yanga SC amesisitiza kuwa kiungo Feisal Salum ataendelea kuitumikia klabu ya Yanga

 

Rais wa klabu ya Yanga SC amesisitiza kuwa kiungo Feisal Salum ataendelea kuitumikia klabu ya Yanga na hakuna namna mchezaji yoyote muhimu kikosini ataondoka katika klabu hiyo.


"Nataka niwahakikishie. Hakuna mchezaji mzuri ambaye ataondoka katika klabu ya Yanga, tufute hiyo kwenye akili zetu"


"Feisal ataendelea kusalia Yanga na tutakaa nae kwa ajili ya kuboresha na kuongeza mkataba wake sio msimu huu ila 2024 baada ya mkataba wake kumalizika"


"Feisal ni mchezaji muhimu kwetu, hakuna uwezekano wa yeye kuondoka. Hilo hatutakubali. Hatusemi hivyo kwa sababu tunataka kutumia nguvu ili abaki, ni kwa sababu tunayo NEGOTIATION POWER.


Amefanya vizuri akiwa na sisi na sisi lazima tumpe thamani anayostahili"

Amesema Rais wa Yanga SC Eng. Hersi Said.

Ads

Post Top Ad

Pages