Post Top Ad

Jumatatu, 2 Januari 2023

Mshambuliaji Cesar Manzoki anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania wiki hii

 


Mshambuliaji Cesar Manzoki anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania wiki hii kukutana na viongozi wa Simba SC kujadili uwezekano wa kuhamia katika klabu hiyo.


Mkataba haukuwa wa moja kwa moja kama ilivyotarajiwa awali, maana klabu anayoitumikia kwa sasa Dalian Pro ya China ilimpa ofa kubwa mchezaji huyo hivyo anatafuta masharti mapya ya kusaini Simba.


Simba inasita kuongezewa masharti mapya kwa sababu Manzoki kwa sasa ana jeraha linalomfanya arejee uwanjani mwishoni mwa mwezi Machi.


Na lengo la Simba ni kumtumia mchezaji huyo katika michezo yake ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika mwezi February mwaka huu 2023.


Manzoki (25) ameonesha nia ya kutaka kuichezea klabu ya Simba SC kwa sasa yupo nchini Uganda.


Ads

Post Top Ad

Pages